tangazo
Habari njema kwa mashabiki wa muigizaji Kajala Masanja ambaye leo hukumu yake
imesomwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au
kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au
kulipa faini ya shilingi milioni 200. Taarifa kutoka mahakamani zinadai
kuwa wasanii wa bongomovie wanachanga fedha hizo ili wazilipe na tayari
inasemekana Wema Sepetu amezitoa fedha hizo zote kutoka mfukoni mwake.
Mrembo huyo na mumewe Faraja Chambo walikuwa wakikabiliwa na makosa
matatu ambayo ni pamoja na kula njama ambapo washtakiwa wote kwa pamoja
walitenda kosa kwa kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala
jijini Dar es Salaam.
Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo
halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha
Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007. Shitaka la tatu
ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda Aprili 14 mwaka 2010 huku
wakijua ni kinyume cha sheria.