tangazo
MAHAKAMA
ya Juu Kabisa nchini Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa
kwa haki kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo, na kutupilia mbali pingamizi
lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura
zilichakachuliwa na mashine za uchaguzi zilijaa kwikwi.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiw kuapishwa wiki ijayo kwenye Machi 9, 2013 hivi.
“Ni
uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nee
walichaguliwa kwa haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga,
akimaanisha Kenyatta na mgombea mwena na Naibu Rais William Ruto
wameshinda kihalali.
Jaji
Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa
kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii,
sekta binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha
umoja, amani, utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.
Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya asilimia 43,28 za Odinga.