Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » "WASANII WAMELAZIMIKA KUTOA PENZI KWA WATOTO W3ADOGO KWA SABABU WANAUME WAMEADIMIKA..." BABY MADAHA

"WASANII WAMELAZIMIKA KUTOA PENZI KWA WATOTO W3ADOGO KWA SABABU WANAUME WAMEADIMIKA..." BABY MADAHA

tangazo

MSANII wa nyimbo za muziki wa bongo fleva  anayefahamika kwa jina la  Baby Madaha amewashukia baadhi ya wasanii wa kike nchini wanaojihusisha na maswala ya ngono na wanaume wenye umri mdogo maarufu kwa jina la 'Kijibwa' kuwa ni hali ya kukata tamaa na ushamba ndio unaochangia kufanya kitendo hiko

Akizungumza jijini Dar es Salaam Msanii huyo alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wasanii hususani wa kike kujihusisha na maswala ya ngono na wavulana wenye umri mdogo huku wakitumia jina la 'kijibwa' kwa ajili ya kukidhi matakwa yao ya kingono

Alieleza kuwa hali ya kukata tamaa ndio chanzo kinachopelekea baadhi ya wasanii hao kujihusisha na maswala ya ngono na vijana wadogo huku wakijipa moyo kuwa wanatafuta faraja wakiwa na vijana hao

"Unajua hao wasichana wanaonekana kukata tamaa kwa kukosa mwanaume wanaolingana kiumri ndio maana ajimchukua mtoto mdogo na kumuhudumia kila kitu na ndipo hapo jina la 'kijibwa' linapotumika kwa kumfananisha mvulana huyo na mbwa unayemuudumia kila kitu huku kazi yake kubwa inakuwa ni kumlinda tu "  aliongezea kuwa

"Kwa sababu mvulana huyo anapewa kila kitu ikiwemo kununuliwa hadi nguo yeye anakuwa na kazi moja tu hivyo hapo hamna mapenzi zaidi ya utumwa na kumsababisha mvulana huyo kukosa uhuru wa kuwa na maamuzi ya mambo yake binafsi" alisema Madaha

Kutokana na hicho kitendo Madaha alikiita ni ushamba kwa kuwa na mahusiano ambayo hayana msingi wowote ule na si kwa ajili ya mtazamo wa maisha hivyo mahusiano hayo hayaendana na mazingira ya nchi na kusababisha kudharaulika kwenye jamii inayomzunguka

Alitoa wito kwa wasichana hao wanaojihusisha na maswala hayo kuwa wanachotakiwa ni kujiamini na kujipanga upya kwa ajili ya kupambana na maisha na kutoyaogopa maisha hivyo wanachotakiwa ni kujipanga upya


PRO-24
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger