tangazo
Watu
watatu wamefikishwa mahakamani katika mikoa ya Kilimanjaro, Dodoma na
Mkoa mpya wa Simiyu kwa tuhuma za kutumia lugha za matusi na uchochezi
dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri yak Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo ASSAH MWAMBENE ameiambia Clouds Fm kwamba watu wawili walikamatwa kwa tuhuma za kumtumia ujumbe mfupi wa maneno wenye lugha za matusi na mmoja alikamatwa na DVD yenye picha za kuhamasisha lugha za matusi kwa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ANNE MAKINDA.
Mapema mwezi uliopita spika MAKINDA alipokea ujumbe mara 400 kwa njia ya simu ya mkononi, pamoja na kupokea simu zote zikiwa na lugha yak matusi, kufuatia namba ya spika kutangazwa hadharani katika mkutano wa chama kimoja cha siasa hapa nchini.