tangazo
Serikali
imewataka Wanawake nchini kuepuka uchochezi wa kidini unaofanywa na
baadhi ya vikundi vya watu pamoja na viongozi wa kidini kutokana na hali
hiyo kuchangia kwa kiasi kikubwa uvunjifu wa amani.
Akizungumza Jijini Dar es salaam, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, SAIDI MECK SADIKI amesema pindi amani inapotoweka wanawake hukabiliwa na wakati mgumu ikiwemo kushindwa kukimbia pindi kunapotokea machafuko katika nchi husika.
MECK SADIKI ameongeza kuwa anataarifa juu ya kuwepo kwa baadhi ya Viongozi wa kidini Jijini Dar es salaam kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambao wanajihusisha na vitendo vya kichochezi kwa lengo la kuvuruga amani iliyopo nchini na kuahidi kukabiliana na viongozi hao. Kwa upande wao baadhi ya Wanawake waliozungumza na Clouds Tv, wamesema umefika wakati kwa Wanawake kote nchini kuhakikisha kuwa wanatumia fursa zilizopo nchini na kulaani watu wanaojihusisha na uchochezi wa kidini nchini.
Wanawake katika mikoa mbalimbali nchini wametumia Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo yameambatana na kauli mbiu isemayo Uelewa wa Masuala ya Kijinsia katika Jamii, Ongeza Kasi, kutoa michango mbalimbali kwa makundi yasiyojiweza pamoja na kujitolea damu ili kupunguza tatizo la uhaba wa damu katika Hospitali mbalimbali nchini.
Pamoja na Serikali kutoa fursa kwa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoa Mikopo kwa Wanawake kila wilaya nchini lakini bado Wanawake wanadai kuwa mikopo hiyo haiwafikii.
Wakizungumza na kituo hiki katika viwanja vya sabasaba Manispaa ya Shinyanga wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, baadhi ya wanawake wamesema kuwa hawaelewi kama kuna kitengo cha kusaidia wakina mama kwenye idara ya maendeleo ya wanawake na watoto.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika siku hiyo ALLY NASSORO RUFUNGA, amesema wananchi watambue kuwa katika Halmashauri kuna fedha zinazotengwa kwa ajili ya kusaidia wakina mama, fedha hizo hazina masharti yoyote wajitokeze kukopa.
Taarifa zinasema kuwa tayari Madaktari wameanza kutibu majeraha na athari zilizotokana na majeraha, ikiwa ni pamoja na kushughulikia uvimbe katika sehemu mbalimbali za kichwa chake na kuondoa damu iliyovilia katika sehemu alizopata majeraha, ili kuwezesha mzunguko wa damu kurudi katika hali yake ya kawaida na kuzuia sehemu nyingine zenye majeraha zisishambuliwe na vijidudu vinavyoweza kusababisha magonjwa mapya.