tangazo
Mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya, Linet Munyali aka Size 8 ametangaza
kuachana na muziki wa dunia baada ya kuokoka.
Kuanzia sasa msanii huyo
atakuwa akiimba nyimbo za injili na leo ameachia video ya wimbo wake wa
kwanza wa gospel, Meteke.
Size 8 ni msanii mwenye mafanikio makubwa nchini Kenya na amekuwa
akitafutwa zaidi kufanya show kuliko msanii mwingine wa kike nchini
humo. Ukimtoa Avril, hakuna msanii mwingine wa kike aliyeweza kushindana
naye.