Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » SHIBUDA ATISHIA KUANDAMANA NA NG'OMBE HADI IKULU.....ANADAI ETI ZINANYANYASWA

SHIBUDA ATISHIA KUANDAMANA NA NG'OMBE HADI IKULU.....ANADAI ETI ZINANYANYASWA

tangazo
Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda anatarajia kuongoza maandamano makubwa ya ng’ombe kutoka Lusumo Nyakabanga Mkoani Kagera, hadi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete ili kupinga uonevu na manyanyaso wanayofanyiwa wafugaji. 
 
“Kama watu wanasema ni porojo za Shibuda, basi wasubiri kama hotuba ya Waziri Mkuu haitakuwa na majibu kwa wafugaji, lazima hayo yatatokea kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, hawa nao ni binadamu waambiwe basi kama hawatakiwi Tanzania,” alisisitiza.
 
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi akiwa na uongozi wa wafugaji kutoka Kanda ya Ziwa ambao wako Dodoma kwa lengo la kuonana na Mawaziri wa Maliasili na Mawaziri wa Mifugo akiwemo Waziri Mkuu, ili kufikisha kilio cha wafugaji ambao wanateketezewa mifugo yao na askari wa wanyama pori.
 
Shibuda alisema kuwa “Katika nchi yoyote duniani hakuna mateso yanayofanywa kwa wananchi wake kama ambavyo inafanyika Tanzania kwa upande wa wafugaji, ni heri ya wakimbizi watakuwa na amani kuliko hawa wanaonekana kama takataka.”
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger