Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , , » VIDEO YA DAYNA NYANGE NA KALA JEREMIAH WAKIWA CHUMBANI SINGIDA YASAMBAA

VIDEO YA DAYNA NYANGE NA KALA JEREMIAH WAKIWA CHUMBANI SINGIDA YASAMBAA

tangazo
MSANII wa vichekesho nchini, Mussa Kitale, amewafanyia umafia wasanii wawili wa muziki, Kala Jeremia na Mwanaisha Said Dayna, baada ya kuwalaza chumba kimoja na kitanda kimoja akiwaambia eti anawafundisha namna ya kucheza filamu.

Picha zilizovuja za Dayna na Kala Jeremia wakiwa mkoani Singida
Hata hivyo, baada ya kufanikiwa kuwapiga picha, alisambaza krip hiyo kwenye baadhi ya mitandao ambapo ilianza kutoa hisia tofauti kwa wadau wa sanaa, wakiamini kuwa wawili hao walikuwa wakifanya ngono katika chumba hicho.

Katika mtandao wa Youtube, watu wengi walikuwa wakiporomosha matusi wakisema kuwa wasanii hao wanataka kutumia ngono kama mbeleko yao ya kuwabeba kisanaa.

Dayna alipoulizwa juu ya tukio hilo la kulala chumba kimoja na Kala Jeremia mkoani Singida, alisema kuwa hawapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, ila Kitale anaandaa filamu ambayo wao watakuwapo kwenye kazi hiyo ya aina yake.

“Ni kweli nasikia mengi mtaani na wengine wanatukana wakisema eti sisi ni wahuni au tupo kwenye mapenzi, ingawa ukweli ni kuwa tupo kwenye filamu zaidi.
“Mimi ni msanii, hivyo kuambiwa nicheze filamu kwangu ni kwepesi zaidi, ndio maana naomba wadau na mashabiki wangu waelewe kuwa sipo kwenye mapenzi na Kala,” alisema.

Hata hivyo Dayna hakuweza wazi ni filamu gani anayocheza na Kala, huku akisema kuwa mwenye uwezo wa kuizungumzia zaidi ni muandaaji mwenyewe Kitale.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger