Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » CHANZO CHA KIFO CHA MSANII ALBERT MANGWEA

CHANZO CHA KIFO CHA MSANII ALBERT MANGWEA

tangazo

Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.

Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. 

Hussein Original ambaye yupo Pretoria amesema Ngwear  na   M to the P  ambaye walikuwa room moja  wamekutwa wamezima   baada  ya  kuzidhisha  madawa  ya  kulevya...

Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi amefariki akiwa usingizini.

Akiongea na mwandishi wetu  muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.


Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka na  kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.

Jonathan  amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi leo nchini.


Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na watu na makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia kwenye mitandao ya kijamii.


Kilimanjaro Lager ‏
Umeondoka wakati bado tasnia ya muziki inakuhitaji. Pumzika kwa Amani Albert Mangwea “Cowwizy”.


Ndovu Special Malt
R.I.P Albert Mangweir! You will be missed by many Tanzanians. 


Adam Nditi
Yani siamini Mangwear amefariki dunia nini ilichomkuta #RIP #Mangwair #akaCowbama


Diva ‏
Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t believe this. I can’t tweet The RIP….. Whyyyyy?

R.I.P NGWAIR 
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger