Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » BREAKING NEWS: KANISA KATOLIKI LALIPULIWA NA BOMU JIJINI ARUSHA WAKATI MISA IKIENDELEA

BREAKING NEWS: KANISA KATOLIKI LALIPULIWA NA BOMU JIJINI ARUSHA WAKATI MISA IKIENDELEA

tangazo

Taarifa  zilizotufikia  hivi  punde  ni  kwamba  bomu  limelipuka  katika  kanisa  katoliki, parokia  mpya  ya Olasisi  iliyokuwa  inazinduliwa  leo  jijini  arusha.....


Bomu  hilo  limelipuka  wakati  waumini  wa  kanisa  hilo  wa  wakijiandaa  na  misa  ya  uzinduzi  wa  parokia  hiyo....
 
Mpaka  sasa  haijajulikana  idadi  kamili  ya  watu  waliojeruhiwa  ama  kupoteza  maisha  lakini taarifa  za  awali  zinasema  kuwa  baadhi  ya  majeruhi  wamekimbizwa  hospitali

Chanzo  cha  mlipuko  huo  inasemekana   kuwa  kuna  gari  ndogo  ilifika  kanisani  hapo  na  kusimama....


Baadae  alishuka  mtu  aliyekuwa  amevalia  vazi  mithili  ya  kanzu  na  kurusha  kitu  kuelekea  kanisani  ambacho  ndicho  kilichosababisha  mlipuko  huo..


Mgeni rasmi   katika  uzinduzi   huo  alikuwa  ni   balozi wa Vatican nchini Tanzania.Yupo  baada  ya kunusurika  katika  mlipuko huo

Hizi ni taarifa za awali tu. Taarifa kamili itawekwa itakapopatikana. Tafadhali endelea kusikiliza Redio Maria Tanzania (inasikika pia online muda huu wakiwa wanatangaza kuhusu tukio hili )
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger