Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » LADY JAYDEE KURIPOTI MAHAKAMANI KESHO

LADY JAYDEE KURIPOTI MAHAKAMANI KESHO

tangazo

MWANAMUZIKI nyota wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kesho (Jumatatu) anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni  kufuatia taarifa alizofikishiwa Meneja na mume wa msanii huyo, Gadna G Habash ‘Captain’.
Gadna alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa Lady Jaydee kufika Mahakama ya Kinondoni, kesho (Jumatatu) Mei 13, mwaka huu.
 

“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni, hii ni baada ya kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo jana na kuleta barua ya kumkabidhi Lady Jaydee mwenyewe japo hawakumkuta” alisema Gadna. 


Katika ukurasa wa Twitter wa Lady Jaydee saa tatu zilizopita aliandika hivi "Sumu ya teja Ukonga, Keko, Segerea. Kesho Mahakamani kizibiti ubaoniii eeeh aaah!" wakati siku ya Ijumaa katika ukurasa wake wa Facebook aliandika hivi: 


"Ratiba ya usiku wa leo ni MACHOZI BAND kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni... Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea... Ila kwa leo mje tuburudike Nyumbani Lounge mpk asubuhi."
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger