Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » "WASANII WA BONGO TUNANYANYASWA"....VICENT KIGOSI

"WASANII WA BONGO TUNANYANYASWA"....VICENT KIGOSI

tangazo

STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amelipuka na kudai kuwa wasanii wa filamu wa Tanzania wanakandamizwa sana na wasambazaji.

Akizungumza na mwandishi wa habari  hii katika mahojiano maalum, Ray alisema: “Kama nitakuwa sijajifunza kitu kutokana na msiba wa Kanumba (Steven) nitakuwa mjinga. Kama utakumbuka, kwenye mazishi yake  serikali nzima ilikuwa pale, umati mkubwa wa watu ulifurika, kwa nini? Kwa sababu ya thamani yake.

“Msambazaji aliye ‘serious’ ni mmoja kwa sasa na yeye ndiye anayeamua cha kufanya na kwa sababu wasanii tupo wengi, hatuna jinsi. Ukiingia naye mkataba unakuwa umeuza haki ya maisha yako yote. Anakuwa na uhuru wa kupeleka DSTV, Zuku na Channel nyingine zozote bila kukulipa chochote.
 
“Lakini mimi siwezi kutupa lawama kwa serikali maana tumeshaongea sana. Nawaomba wadau wajitokeze wawekeze kwenye tasnia yetu maana inapanuka na ina soko kubwa ila msambazaji yupo mmoja tu ndiyo maana tunanyonywa.”

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger