Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » HUU NI UJUMBE ALIOTUMA MTANZANIA MWENZETU AMBAYE AMEFUNGWA ANGOLA BAADA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA

HUU NI UJUMBE ALIOTUMA MTANZANIA MWENZETU AMBAYE AMEFUNGWA ANGOLA BAADA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA

tangazo

Baadhi ya ndugu na marafiki wa Mtanzania aliehukumiwa kifungo cha miaka nane nchini Angola baada ya kupatikana na dawa za kulevya alizokua akizisafirisha kwenda Afrika Kusini, wamepaza sauti kuomba msaada wa Serikali ili ndugu yao aje kufungiwa gerezani Tanzania.

Khaleed Bin Abad amesema huyu Mtanzania aliondoka South Afrika na kwenda kufata dawa za kulevya Brazil na akafanikiwa kuchukua ila wakati anarudi Afrika Kusini kwenye kubadilisha ndege Angola alikamatwa na kukutwa na dawa za kulevya miaka mitatu iliyopita.

Kwa kipindi chote hicho huyu jamaa amekua akishikiliwa Angola bila kujua hatma yake na hata kushindwa kukutana na balozi wa Tanzania Angola lakini wiki mbili zilizopita ndio amehukumiwa kifungo cha miaka 8.

Ombi lililoambatana na ndugu hawa kupaza sauti, ni kuiomba serikali kusaidia mtu huyu kukutana na balozi wa huko ili utaratibu wa kuja kufungwa Tanzania ujulikane.

Mara nyingi Mtanzania huyu amekua akituma msg kwa kutumia simu za watu wengine aliokutana nao gerezani.


MillardAyo
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger