Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MWANAMKE AFUNGWA MIAKA 3 KWA KOSA LA KUMNG'ATA MUMEWE SEHEMU ZA SIRI HUKO IRAMBA SINGIDA

MWANAMKE AFUNGWA MIAKA 3 KWA KOSA LA KUMNG'ATA MUMEWE SEHEMU ZA SIRI HUKO IRAMBA SINGIDA

tangazo

MAHAKAMA ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida umemhukumu mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Kisana wilayani humo, Sayuni Ramadhani (42) kwenda jela miaka mitatu baada ya kukiri kosa la kumng’ata mumewe sehemu zake za siri.

Mwendesha mashitaka mkaguzi wa polisi, Vincent Ndasa alidai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Iramba, Kariho Mrisho kuwa Juni 4 mwaka huu saa 12.00 jioni katika kijiji cha Kisana, mshitakiwa kwa makusudi alizing’ata kwa meno sehemu za siri za mume wake, Onesmo Nathania (42) na kumsababishia maumivu.

Ndasa alidai kuwa siku ya tukio, wanandoa hao waliporejea nyumbani kutoka kwenye klabu cha pombe ya kienyeji kijijini hao, kulitokea kutokuelewana na hivyo kuanza kugombana.

Alidai wakati wanaendelea kupigana, Onesmo alizidiwa nguvu na kuangushwa chini na mkewe ambaye alifungua zipu ya suruali na kufanikiwa kuzitoa sehemu za siri za mumewe na kuzing'ata nusura azitenganishe.

Mwendesha mashitaka aliendelea kudai kuwa mlalamikaji Onesmo alipiga yowe na majirani walifika mara moja na kumkimbiza katika zahanati ya kijiji kwa ajili ya matibabu.

Mshitakiwa alipoulizwa iwapo ni kweli alikiri kosa na akaiomba mahakama imwonee huruma kwa kumpa adhabu ndogo kwa kuwa hilo lilikuwa ni kosa lake la kwanza na kwamba anahitaji kuwa na mumewe ili waendelee kulea idadi kubwa ya watoto wao kwa pamoja.

Naye mwendesha mashitaka, Ndasa aliiomba mahakama kumpa adhabu kali mshitakiwa ili kuwa fundisho kwake na pia kuogofya wanawake wanaotarajia kuwafanyia unyama wa aina hii ya kung’ata sehemu nyeti za waume zao.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Mrisho, alisema mahakama yake imezingatia kwa makini maombolezo ya mshitakiwa na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kutumikia jela miaka mitatu.

Source:habari leo
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger