Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » SUMATRA KUBURUZWA MAHAKAMANI BAADA YA KUPANDISHA NAULI ZA MABASI NA DALADALA KIHOLELA

SUMATRA KUBURUZWA MAHAKAMANI BAADA YA KUPANDISHA NAULI ZA MABASI NA DALADALA KIHOLELA

tangazo


Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kimesema kinaiburuza kortini Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (SUMATRA), kwa madai kuwa hakikushirikishwa kwenye mchakato wa kuongeza nauli za abiria.
Aidha, CHAKUA kimeitaka serikali kuuwajibisha uongozi wa juu wa SUMATRA kwa kuifuta na kuunda upya kwa madai kwamba imeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi wanyonge.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mshauri wa chama hicho, Wilson Mashaka, alisema tangazo la kupandisha nauli halikujengwa kwa dhana ya ushirikishwaji, kwani vikao vilivyofanyika kati ya Septemba na Novemba, 2012, vilifanyika kwa kuwashirikisha wamiliki wa mabasi lakini wadau muhimu kama CHAKUA hawakushirikishwa.

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger