Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » "SIKU YA MAZISHI YANGU WATAJAA WATOTO NA MASHOGA TU"....AUNT LULU

"SIKU YA MAZISHI YANGU WATAJAA WATOTO NA MASHOGA TU"....AUNT LULU

tangazo

MSANII wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa siku akifa anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na mashoga pamoja na watoto.

Akizungumza na mwandishi  wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema kutokana na ukweli kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto waliokuwa wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio One na ITV na mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo watakaojaa kwenye mazishi yake.


Alisema sababu kubwa ya msiba wake kujaa mashoga wengi ni kwa kuwa kabla hajabadili mfumo wa maisha anayoishi sasa, alikuwa akiwalea hivyo siku ya mazishi lazima wakumbuke fadhila.

“Unajua kufa ni kama kulala, naamini siku ya mazishi yangu watakaokuwa wengi ni watoto pamoja na mashoga ambao zamani nilikuwa mama yao, wengine ni waandishi na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki,”alisema Aunty Lulu.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger