Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » DHARAU ZA PAUL KAGAME KWA USHAURI WA RAIS KIKWETE .....

DHARAU ZA PAUL KAGAME KWA USHAURI WA RAIS KIKWETE .....

tangazo
 

DHARAU  za Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jakaya Mrisho Kikwete zimewagawa Watanzania  na  kuwafanya  wawe  na  mitazamo  tofauti.


Wapo  wanaomuunga  mkono  Rais  Kagame  na  wapo  pia  wanaompinga  kwa  kauli  yake...


Rais Kagame alimkejeli  Rais Kiwete kwa kuuita ushauri wake ni ushauri wa kijinga kwa wanyarandwa,awali Rais Kikwete alizishauri nchi za Rwanda na Congo DRC kukutana na kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani.

Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati wa mkutano wa kujadili amani na mpango wa ulinzi nchini Congo DRC uliofanyika katika Makao Makuu ya AU mjini Addis Ababa Ethiopia.

Katika ushauri huo Rais Kikwete alisema kwamba ni vyema Rais Kagame akakaa katika meza ya mazungumzo ya amani na Rais wa Congo DRC Joseph Kabila ili kumaliza tofauti zao badala ya kutumia nguvu ya kijeshi.

“Nimekaa kimya kwa kipindi kirefu na kwa jinsi nilivyoweza kwa sababu nilifikiri kwamba mazungumzo ya kipuuzi yaliyozungumzwa na watu wajinga yamemalizika "alisema Rais Kagame.

Katika hatua nyingine Rais Kagame alisema kwamba ushauri huo wa Rais Kikwete ni sawa na kuwachezea wanyarandwa mbele ya mataifa.  

Rais Kagame aliyasema hayo katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya maofisa wa jeshi wapatao 45 katika kituo cha mafunzo ya kijeshi siku ya Juma Tatu nchini Rwanda.

NB:
RAIS  WETU  SIYO  MJINGA... HILO  NI  TUSI , JK ALIWAPA  USHAURI  WA  BURE...MLIKUWA  HURU  KUUTUMIA  AU  KUUACHA

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger