Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MSHIRIKI WA TANZANIA ( NANDO ) ATIMULIWA BIG BROTHER BAADA YA KUGOMBANA NA MSHIRIKI MWENZAKE

MSHIRIKI WA TANZANIA ( NANDO ) ATIMULIWA BIG BROTHER BAADA YA KUGOMBANA NA MSHIRIKI MWENZAKE

tangazo
Jana usiku mara tu baada ya Sulu na Annabel kutolewa kwa kura za watazamaji, Big Brother aliwaita washiriki pamoja katika kikao cha dharura kufuatia ugomvi uliotokea kati ya Nando na Elikem.

Itakumbukwa kwamba siku ya ijumaa ilitokea hali ya kutoelewana kati ya Nando na Elikem. Wawili hawa walitukanana sana na kutishiana mno. Ugomvi huo ulianzishwa na Nando.

Kwa mujibu wa sheria za Big Brother mwaka huu, kuanzisha ugomvi ni kosa ambalo hupelekea kupata 'strike' ama onyo.

3 strike rule ni mtindo unaotumika msimu huu. Kwa mujibu wa Big brother, yeyote atakaye fanya makosa matatu makubwa na kupewa maonyo matatu basi moja kwa moja anatakiwa atimuliwe..

Sheria hiyo imetumika kumtimua Nando kwa sababu 1. Alianzisha ugomvi siku ya Ijumaa, 2. Alishiriki ugomvi na Elikem na 3. Alitishia maisha, "I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die"...

Katika kipindi cha wiki 9 za ushiriki wake katika jumba hilo, Nando amekutwa na misuko suko kadhaa ikiwemo kuwahi kukutwa na kisu katika Party ya Channel O pia kukutwa na mkasi chini ya kitanda kitu ambacho ni kinyume cha sheria za big brother.

Kutokana na ugomvi huo Elikem alipata strike moja.

Big brother alimtaka Nando aondoke katika jumba lake hilo na kutumia fursa hiyo kuwataka washiriki wengine waishi kama watu wazima.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger