Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » JE, HARUSI YA AL QAIDA NA JAMSHID ITAWEZA KUTIMIZA NDOTO ZAO?

JE, HARUSI YA AL QAIDA NA JAMSHID ITAWEZA KUTIMIZA NDOTO ZAO?

tangazo

Mauaji ya Mombasa na pwani ya Kenya, yaliyotokea hivi karibuni, na yale yale ya Zanzibar siku chache kabla yanaonyesha wazi kuwa kuna mkono wa Jamshid nyuma yake. Mbinu zinazotumika ni chinja chinja ya Al-Qaeda yakuua watu wasio na hatia ili kutisha wengine wale walio na moyo hafifu waseme tuwaachie …

Jamshid na wapambe wake wamekuwa wakidai kwa muda mrefu sasa kuwa wangetaka kurudisha ukoloni wa Waarabu Zanzibar na pwani ya Afrika Mashariki na ili kufanikisha lengo hilo wanatumia mbinu za Al-Quaeda za kujenga chuki kati ya Uislam na dini nyingine au kabila moja dhidi ya kabila lingine. Lengo la kutafuta dini au kabila la kulengeshea chuki ni ili kuwalaghai watu wengine kuwa wanatetea maslahi yao wakati ukweli ni kwamba wanataka tu kufikia malengo yao ya utawala wa wachache kwa kuwapanda mgongoni mwa wengine ...


Pwani ya Kenya wanadai kuwa ni Wadigo wanataka kujitenga na Kenya ili waunde Jamhuri yao ya Mombasa. Zanzibar wanahamasisha chuki dhidi ya Ukristu ili kulaghai Waafrika walio Waislam kuwa wako katika jahazi moja na wale wanaotaka kurudisha utawala wa Jamshid kwa madai kuwa ni Mwislam kama wao. Hii licha ya ukweli kuwa Zanzibar, kwa muda mrefu imekuwa ikiongozwa na Mwislam.


Jamshid sasa hivi ana umri wa karibu miaka 84 na ijapokuwa alipigwa marufuku huko Zanzibar mwaka 1964, hiyo marufuku ilikuwa lifted mwaka 1999 na Rais wa Zanzibar wakati huo Salmin Amur na kwamba tangia hapo ilikuwa ruksa kwa Jamshid kurudi Zanzibar kama raia wa kawaida. Lakini Jamshid na wapambe wake hawakutaka kurudi Zanzibar kama raia wa kawaida bali walitaka kurudisha utawala wa Waarabu wachache kama ilivyokuwa kabla hawajaondolewa madarakani.


Ijapokuwa Jamshid ana miaka hiyo 84 na huenda nguvu zake za mwili na akili zinamwishia, ana watoto wa kiume watano na wa kike wawili wernye umri kati ya miaka 57 na 38, na mmoja au zaidi ya hawa aweza kuwa ndiye anatumaini kuwa chinja chinja ya ki-Al-Qaeda itaiwezesha familia ya Jamshid kufanikiwa katika malengo yao.


Inabidi kieleweke kinachoendelea ni nini. Idadi ya Waarabu wakazi wa Zanzibar haizidi 4,000 wakati Waafrika ni zaidi ya millioni. Kwa hiyo wanataka kurudisha utawala wa wachache juu ya wengi mfumo ambao umepigwa vita na kuondolewa dunia nzima.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger