Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MWAKTEMBE AWAFUKUZA KAZI WALIOMSAIDIA AGNESS MASOGANGE KUPITISHA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE

MWAKTEMBE AWAFUKUZA KAZI WALIOMSAIDIA AGNESS MASOGANGE KUPITISHA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE

tangazo

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kuwafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agness Gerald na mwenziye Mellisa Edward kupitisha dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine "TIK" au "Meth" au "USAN" kilogramu 180 kuelekea Afrika Kusini Julai 5, ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha O. R. Tambo nchini humo.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya.


Waliofukuzwa ni   Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed ambao walihusika katika kuwasaidia Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger