Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI wasitisha MAANDAMANO yaliyopangwa kufanyika kesho

CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI wasitisha MAANDAMANO yaliyopangwa kufanyika kesho

tangazo

Vyama vitatu vya Upinzani vinavyounda Umoja wa vyama vya Upinzani nchini vilivyopanga kufanya maandamano ya amani kupinga baadhi ya vipengele vilivypopo kwenye rasimu ya katiba vimeridhia kuahirisha maandamano hayo yaliyokuwa yafanyike Septemba 21 mwaka huu.

Vyama hivyo ambavyo ni CUF,CHADEMA,na NCCR MAGEUZI kwa pamoja vimekubaliana na uongozi wa juu wa jeshi la Polisi nchini kusitisha maandamano hayo ili kuepusha shari za Kiusalama ambazo zingeweza kutokea kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizobainishwa na jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP SAID MWEMA amesema jeshi hilo limeridhia vyama hivyo kufanya Mkutano wa hadhara Septemba 21 mwaka huu jijini Dar es Saaam na kwamba dhamana ya ulinzi wa Mkutano huo itakuwa chini ya Jeshi hilo.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger