Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Meli ya Tanzania yakamatwa na madawa ya kulevya Italia...

Meli ya Tanzania yakamatwa na madawa ya kulevya Italia...

tangazo

MV Gold Star ikiungua baada ya kuchomwa moto na wasafirishaji wa madawa ya kulevya.

Moshi mkubwa ukitoka katika meli hiyo baada ya wahusika kujitosa majini.MV Gold Star ikipelekwa katika Bandari ya Sicilia.
 
-NI MV GOLD STAR -WATUHUMIWA WAICHOMA MOTO KUPOTEZA USHAHIDI, WAJITOSA MAJINI -ILIKUWA NA DAWA ZA KULEVYA ZENYE THAMANI YA BILIONI 126.5 -MZIGO ULIOKUWEMO NI TANI 30 ZILIZOKUWA  ZINAPELEKWA UTURUKI -9 WAKAMATWA, NI RAIA WA MISRI NA SYRIA

MELI iliyosajiliwa nchini Tanzania ya MV Gold Star juzi Ijumaa imekamatwa nchini Italia ikiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya pauni milioni 50 sawa na shilingi bilioni 126. 5. Watuhumiwa waliokuwa ndani ya meli hiyo waliamua kuichoma moto ili kupoteza ushahidi na kuamua kupiga mbizi majini lakini walitiwa nguvuni na wanausalama wa Italia.

Meli hiyo ya mizigo ilikuwa imepakia tani 30 za madawa na ilikamatwa jirani na Kisiwa cha Sicilia katika Bahari ya Mediterranian nchini Italia wakati ikielekea Uturuki. Maofisa wa polisi nchini humo wamedai kuwa watuhumiwa tisa waliokamatwa ni raia wa Misri na Syria na watafikishwa mbele ya sheria. Moto katika meli hiyo umezimwa na tayari imepelekwa katika Bandari ya Sicilia.



HAPA CHINI NI VIDEO WAKATI MELI HIYO IKIUNGUA:


Source: Daily Mail
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger