Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Picha tano za yule daktari FEKI aliyenaswa katika hospitali ya KCMC

Picha tano za yule daktari FEKI aliyenaswa katika hospitali ya KCMC

tangazo
  
 Daktari feki aliyenaswa katika hosptali ya KCMC aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo.
Daktari Feki akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa 'akihudumia'.
Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo (kushoto) akimwonesha Daktari Feki, Alex Massawe.
Daktari Feki akiwa katika gari la polisi tayari kupelekwa kituoni.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, jana ulimnasa 'Daktari Feki' aitwaye Alex Sumni Massawe (33).
Massawe alikamatwa saa 5:00 asubuhi ndani ya hospitali hiyo na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amepanga kumfanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa malipo ya Sh. 200,000.

Habari zinasema kuwa kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana huyo, mkazi wa Manispaa ya Moshi, Pamvelina Shirima, alikutana na mtuhumiwa huyo katika baa moja maarufu iliyopo eneo la Dar Street (jina limehifadhiwa) na kumtaka ampe kiasi hicho cha fedha kwa madai zitatumika kuharakisha mwanaye wa kiume kufanyiwa vipimo vya upasuaji.

Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo, alisema kuwa daktari huyo aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo baada ya baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mtu ambaye amekuwa akijitangaza kwamba ni daktari.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger