Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Mwanaume aua watu wawili na kisha kujiua yeye mwenyewe kwa risasi jijini Dar leo

Mwanaume aua watu wawili na kisha kujiua yeye mwenyewe kwa risasi jijini Dar leo

tangazo
 
Mtu mmoja aliyefahamika  kwa  jina   la  Gabriel  Munisi   ambaye  ni  mfanyabiashara  toka  jijini Mwanza  amewaua watu wawili kwa kuwapiga risasi ndani ya gari na kujeruhi mmoja kisha naye akajiua kwa risasi leo asubuhi  jirani na Baa ya Wazee iliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam!
 
Inadaiwa  kuwa   waliouawa  walikuwa  ndani  ya  gari wakitoka  getiini .Ndani  ya  gari  hiyo kulikuwa  na dereva mwanaume, abiria mwanamke mbele, na abiria wengine wawili wakiwa siti  ya nyuma.
 
Nje  kidogo  ya  geti  kulikua na jamaa kasimama. Inadaiwa alishushwa hapo dakika chache toka katika tax..Walipotokeza abiria hao kupitia gari yao, jamaa  huyo alitoa silaha yake na kupiga risasi gari akilenga zaidi abiria wa mbele pande zote kisha na nyuma. Baada ya kumaliza hapo muuaji huyo naye alijipiga risasi na kufariki hapo hapo.
 
Dereva na abiria wake wa mbele wamefariki dunia, huku abiria wa nyuma mmoja mama mtu mzima kajeruhiwa na risasi mgongoni na dada mwingine kajeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger