Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Nape Nnauye amtaka msajili wa vyama vya siasa aikifute chama cha CHADEMA kwa madai kuwa kimeshindwa kusimsmia katiba yake

Nape Nnauye amtaka msajili wa vyama vya siasa aikifute chama cha CHADEMA kwa madai kuwa kimeshindwa kusimsmia katiba yake

tangazo
 
Songea.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kukifuta Chadema kwa madai kuwa, kimeshindwa kusimamia katiba yake kwa kutofanya uchaguzi wa ndani zaidi ya miaka zaidi ya kumi.
 
Nape alisema chama hicho kimejaa viongozi waongo, wapenda vurugu na wanaotaka kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha Katiba Mpya na kwamba, wamesahau katiba iliyopo imedumu kwa miaka 50 na haijawahi kuwagombanisha wananchi wala kuwavuruga.
 
Hata hivyo, jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika kuzungumzia tuhuma hizo jana jioni kwa simu yake haikufanikiwa.
 
Akihutubia wakazi wa Manispaa ya Songea jana, Nape alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kukiagiza chama hicho kufanya mkutano wa uchaguzi haraka kikigoma akifute na kwamba, asipofanya hivyo wao wataendelea kumsema na kumchukulia hatua.
 
Aliongeza CCM kilifanya uchaguzi wake 2012 na kupata viongozi wapya, lakini Chadema imeshindwa kusimamia katiba yake ambayo ilipeleka kwa msajili wa vyama na kuisajili kwa kuivunja wao wenyewe kwa kuendesha chama isivyo.
 
Nape alisema chama hicho hakifai kuongoza nchi, kwani kimeshindwa kusimamia katiba yake na kuifuata hakiwezi kuongoza wananchi.
 
“Kwa sababu Msajili wa Siasa ni mlezi wa vyama vyote vya siasa ikiwamo Chadema, namuomba akiagize chama hicho kifanye uchaguzi kwani wao wanajiita wanademokrasia wakati wanashindwa kufuata demokrasia kwa vitendo,” alisema Nape.
 
Kuhusu malalamiko ya wananchi, Nape alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi wa Serikali na kwamba, yana msingi kwani inasikitisha licha ya Ruvuma kuwa ni mkoa unaolisha nchi, hakuna mawazili wa kilimo ambao wamefika mkoani hapa.

-Mwananchi
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger