Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Showing posts with label Rihanna. Show all posts
Showing posts with label Rihanna. Show all posts

RIHANNA NA CHRIS BROWN WAFIKIRIA KUPATA MTOTO


Wiki kadhaa baada ya kurudiana, huenda Rihanna na Chris Brown wakaupeleka uhusiano wao mbele zaidi kipindi hiki, kwa kuwa na familia na watoto.
 



Rihanna ameliambia jarida la ELLE UK kuhusu mwanzo mpya wa mahusiano yake na Chris.Kuhusu mipango ya kuwa na watoto anasema:

“Bila shaka ntakuwa na mtoto. Na nasali niweze kwenda mapumziko kwa mwezi mmoja mzuri. Na nimejiwekea mambo fulani hivyo sina haja ya kufanya tour katika maisha yangu yote yaliyobaki hata kama napenda kufanya tour. 

Nataka afya na furaha katika miaka mitano. Nataka kuwa mwenye afya na mwenye furaha.”

TUPE MAONI YAKO

RIHANNA AMTEGA MLINZI WAKE


 Muimbaji asiyeishiwa  vituko Rihanna ameonekana kumtega mlinzi wake kwa kivazi alichotinga kilichomuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake

Rihanna aliweza kugundua hilo na ndipo alipoamua kuanza kuishusha nguo yake 'gauni' lililokuwa linaonekana kupanda huku likiachia sehemu kubwa ya mwili wake

Rihanna ambaye ameanza kuizungumzia nyimbo yake ya 'Unapologetic', akiwa ameanza kufanya video shoot ameonekana akiwa amevaa gauni fupi jeusi

TUPE MAONI YAKO

RIHANNA ATAJA SABABU ZILIZOMFANYA ARUDISHE PENZI LAKE WA CHRISS BROWN


Rihanna amefunguka mengi kuhusu uhusiano wake na Chris Brown na kuweka wazi kwanini aliamua kumpa second chance.


“Niliona  ni muhimu zaidi kwa mimi kuwa na furaha, “ aliliambia jarida lijalo la Rolling Stone. “Sikutaka kuacha mtazamo wa mtu yeyote hata kama ni kosa, ni kosa.”

Katika toleo hilo litakalotoka kesho, Rihanna ameelezea vitu vilivyobadilika kati yao.

“Unatuona tukitembea sehemu, tukiendesha sehemu, tukiwa studio, tukiwa club, na unadhani unajua. Lakini ni tofauti sasa. Hatuna majibizano kama ya zamani tena. Tunaongea kuhusu mambo. Tunathaminiana. Tunajua fika tunachokataka sasa na hatutaki tukipoteze.”
TUPE MAONI YAKO
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger