Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimemvua madaraka ya uongozi Dr. Kitila Mkumbo kwa madai ya kujihusisha na uongozi wa vyama vya siasa

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimemvua madaraka ya uongozi Dr. Kitila Mkumbo kwa madai ya kujihusisha na uongozi wa vyama vya siasa

tangazo
 
\Taarifa zinasema kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umemvua kwa muda Mhadhiwa Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo madaraka ya kuongoza Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE).

Hatua hiyo inatajwa kuchukuliwa baada ya uongozi wa UDSM kupata taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa Dk Kitila Mkumbo alikuwa kiongozi wa chama cha siasa, CHADEMA wakati angali ni mtumishi wa umma, jambo ambalo Uongozi wa chuo hicho umekariri kuwa ni kinyume cha sheria ya nchi na Serikali kwa mfanyakazi wa umma kushika wadhifa katika chama cha siasa.

Kutokana na uamuzi wa chuo hicho, Dk Kitila aliandikiwa na kukabidhiwa barua ya kusimamishwa kwake wadhifa huo.

Dk Kitila bado ataendelea kuwa Mhadhiri Mwandamizi kwenye kitivo hicho
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger