tangazo
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefarijika kuona hali nzuri walizonazo mastaa wenzao walioko Segerea, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Kajala Masanja.
Taarifa tulizozipata zinasema, Jumamosi iliyopita Amanda na mwigizaji Husna Poshi ‘Dotnata’ waliambatana kwenda kuwajulia hali mastaa hao ambao wapo nyuma ya nondo wakikabiliwa na kesi tofauti.
Imeelezwa kuwa Lulu na Kajala walifarijika kuwaona mastaa hao ambapo waliwaombea kwa Mungu ili kesi zao ziende haraka waweze kurudi uraiani.