Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Showing posts with label LULU MICHAEL. Show all posts
Showing posts with label LULU MICHAEL. Show all posts

Lulu Michael ndani ya MKASI SHOW....Safari hii atatudanganya nini??...Hizi ni picha tano za maandalizi

 
Actress Lulu  Michel  is so busy nowadays shooting new movies, media interviews and many more. Today the Swahili movies screen queen was on set shooting her interview with Mkasi Tv show which is aired on East Africa Television..

Kaa tayari kwa vipindi vya Mkasi Vinavyofuata kujua Lulu aliongelea nini. Je Safari hii atatudanganya MIAKA  TENA??
 
 
 
 


TUPE MAONI YAKO

"SASA NIMEOKOKA.....UJINGA SITAKI TENA"...LULU MICHAEL


MUIGIZAJI machachari wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema baada ya kupata misukosuko ya kimaisha, sasa maisha yake ameyaelekeza katika sala kumuomba Mungu amsamehe makosa yake. 


Lulu alisema hayo juzi, katika kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha Jijini Dar es Salaam.

“Sasa hivi nasali sana, namuamini Mungu katika maisha yangu na mbali ya kwenda kanisani, pia nasali mwenyewe katika sala zangu.

“Ningependa maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini yote ya Mungu labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja kuyaishi baadaye,” alisema Lulu.

Katika hatua nyingine, alisema anavutiwa na kazi ya msanii wa bongo fleva, Bernard Paul ’Ben Pol’ ambaye tungo za nyimbo zake zinamkosha kuzisikiliza.

TUPE MAONI YAKO

"GEREZANI KUMENIFANYA NIMJUE MUNGU VIZURI SANA"....HII NI INTERVIEW YA LULU MICHAEL



Kwa mara ya kwanza muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu jana alifanya interview ya kwanza tangu atoke gerezani January mwaka huu. 

Lulu aliye na muonekano wa ‘udada’ zaidi alihojiwa jana kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema.
 Katia interview hiyo, Lulu aliongea masuala mengi kuhusu maisha yake ya sasa, mipango yake na mengine lakini akidai kuwa hatopenda kuongelea suala la uhusiano wake na Kanumba kwakuwa anahisi bado hajawa tayari ila muda ukifika atafunguka mengi. Haya ni baadhi ya masuala aliyoyazungumza.

Kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya Foolish Age


Ninaplan kufanya uzinduzi kwaajili ya movie yangu, lengo kubwa la kufanya uzinduzi ni kwamba kwanza nitajiskia vizuri kukutana na ‘okay these are my fans’ kukutana nao sehemu moja. Kuna vitu sitaweza kuongea kwenye interview ntahitaji kuviongea mwenyewe kama mwenyewe. 



Nitahitaji watu waone baadhi ya vitu vilivyopo kwenye movie. Movie inaitwa Foolish Age. Nitaizindua chini ya kampuni ya Proen (????) Promotions Ltd na ni kampuni ambayo ndio inanimanage kwa sasa.

Kuhusu kama ana boyfriend aliyemnunulia vitu vya thamani

Watanzania wengi tulishajiwekea ile dhana kwamba ‘ukiona mwanamke amefanya kitu basi there is a man behind, yaani ni ile dhani ipo tayari ndani yetu kwahiyo hata kama mtu atastruggle kutafuta kitu chake mwenyewe lakini hiyo itakuwa ni ukweli wako na unaujua mwenyewe . 



Kiukweli ni kwamba hakuna mwanaume yeyote ambaye amenifanyia chochote till now. Nachoshukuru tu ni menejimenti yangu, kampuni ambayo nafanya nayo kazi.


 Ni kampuni ambayo inanijali, inajali kazi zangu, inajali msanii wao kwahiyo whatever I’m having, whatever I’m doing ni mimi mwenyewe, ni kazi zangu ni biashara yangu.

Uhusiano wake na Mama Kanumba na jinsi alivyompata kufanya naye movie ‘Mapenzi ya Mungu’

Kwa sasa hivi tupo kama familia kwa hiyo it wasn’t hard mimi kumpata na nilijisikia vizuri kama ntaweza kufanya naye kazi. Kuna spirit ambayo ilinivuta zaidi nifanya kazi na Mama Kanumba kuliko labda mama mwingine.

Anachomiss kwa Kanumba

Busara zake, he was a person ambaye akikuona unaenda hivi he takes you in the right way.

Kuhusu kwanini mapenzi yake na Kanumba yalikuwa siri
Ni makubaliano tu and there was no need like to let people know yaani kumfanya kila mtu ajue nadhani haikuwa na maana kwetu.

Kuhusu kwanini alinenepa alipokuwa gerezani


Labda kwasababu nilimwachia Mungu kila kitu, nilimkabidhi Mungu kila kitu so I had this peace of mind. Niliacha kwamba yeye ni msimamizi wa kila kitu. Let me confess kwamba gerezani kumenifanya nimjue Mungu vizuri sana,. 



Kumenifanya nimjue na nimwamini na kumjua na kumwamini kumetokana kwamba kuna vitu vingi vimekuwa vinafanyika like naviona hivi kwa macho na naona kabisa kwamba hapa ingekuwa mimi kama mimi ama binadamu yeyote haiwezekani...

So ni Mungu tu ndio ameweza kufanya hili likapita. Kwahiyo niliamua tu kumwachia yeye kila kitu nikajikuta tu nina amani.

MSIKILIZE HAPO CHINI

TUPE MAONI YAKO

VIGOGO WA DUBAI WAMGOMBANIA LULU MICHAEL ....


HABARI zilizonaswa na mwandishi  wetu  zinaeleza kuwa nyota wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameitwa katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kwa ajili ya kula  bata ikiwa ni pole yake kwa kusota Gereza la Segerea kwa karibu mwaka mmoja.

Chanzo kimoja  kilipenyeza habari kuwa mapedeshee hao wamemualika staa huyo huku ikinyetishwa kwamba, vigogo wa sanaa hiyo Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ndiyo watakaomsindikiza.
 

“Mapedeshee wamemtumia mamilioni ya fedha Lulu, wanataka kufanya naye pati ya pamoja kwa vile ni miongoni mwa mastaa wa Bongo wanaokubalika nchini humo na pia kumpa pole kwa kukaa gerezani muda mrefu.
 

“Mbali na sherehe hiyo, watakapokuwa nchini humo wanatarajia kuendeleza filamu ambayo wameanza kuirekodi hapa Bongo,” kilisema chanzo hicho.
 

Hata hivyo, chanzo kiliweka wazi kwamba kwa sasa, Lulu si rahisi kusafiri nje ya Bongo kwa vile kesi aliyonayo ina mipaka ya sehemu za kwenda.
Alipotafutwa Dk. Cheni juu ya ishu hiyo, alisema waliomuita Lulu si mapedeshee bali ni Wabongo waishio kule, lakini masharti ya kesi yake hawezi kusafiri nje ya Tanzania.
Dk. Cheni akaulizwa kuhusu yeye na Steve Nyerere kuwepo kwenye safari hiyo ambapo alisema hana ufafanuzi zaidi, akakata simu.
TUPE MAONI YAKO

"SIONI TATIZO KWA LULU MICHAEL KUPIGA PICHA NA PENNY....HUO NI UMBEA WA MAGAZETI"..WEMA SEPETU


Hivi  karibuni  zilisambaa  picha  za  Lulu  Michael  akiwa  katika  picha  ya  pamoja  na  Penny....

Picha  hizo  zilizua  utata  mkubwa  miongoni  mwa  watu  huku  kundi  kubwa  likidai  kuwa  picha  hizo  zimepigwa  makusudi  kwa  lengo  la  kumuumiza  Wema  Sepetu...
 Lulu Michael  akiwa  na Penny

Madai  hayo  yaliandikwa  kwa  kina  na  gazeti  moja  la  udaku  hapa  nchini  likisimulia  ugomvi   uliopo  kati  ya Penny  na Wema Sepetu.....

Waswahili  husema:
             Kama  A=B   na    B=C    basi   C= A  pia...!!!! 

Huo  ndo  ulikuwa  mtazamo  wa  gazeti  hilo  kusuhu  ukaribu  wa  Penny  na Lulu Michael.....

Akizijibu  tuhuma  hizo,Wema  Sepetu  ameamua  kuvunja  ukimya  na  kudai  kuwa  hawezi  kuwa  na  beef  na  baby  wake  Lulu  kwa  sababu  ya  Penny.....

Huu  ndo  ujumbe  wake



TUPE MAONI YAKO

"WANAOSEMA NIMEZEEKA IMEKULA KWAO....LEO NDO KWANZA NIMEFIKISHA MIAKA 18"...LULU MICHAEL

Leo  Elizabeth Michael  ametimiza  miaka  18.....Anadai  kuwa  wanaodai  kuwa  amezeeka  imekula  kwao  maana  ndo  kwanza  anauanza  utu  uzima





























TUPE MAONI YAKO

LULU MICHAEL ALILIA PENZI LA STEVEN KANUMBA.....

Wakati zikiwa zimebaki wiki chache tu hadi kifo cha Stephen Kanumba kitimize mwaka mmoja, aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael aka Lulu kwa mara ya kwanza leo ameandika ujumbe kuhusiana na jinsi anavyomkumbuka.


Lulu aliachiwa kwa dhamana mwezi January mwaka huu baada ya kukaa mahabusu kwa takriban miezi minane kufuatia kukamatwa kwa kuhusika na kifo cha Kanumba.
Lulu ambaye hivi karibuni amekuwa akitweet mara kwa mara ameandika:

“Ulikuwa zaidi ya baba,kaka,mpenzi,mume,ndugu,rafiki….sitoacha kukulilia katika maisha yangu yote!!R.I.P daddy angu STEVEN KANUMBA.”

Akiambatanisha na picha ya Kanumba, Lulu ameongeza, “I will alwayz love u daddy angu!”



Unaweza kumfollow Elizabeth Michael ‏Twitter kwa jina la @hotlulumichael.

TUPE MAONI YAKO

NIMEMALIZA KWA LULU NAHAMIA KWA KAJALA"..DK. CHENI


STAA aliyekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ anapata dhamana, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amefunguka kuwa baada ya kufanikiwa kwa Lulu sasa anahamia kwa msanii mwingine, Kajala Masanja.     

Akizungumza nje ya Mahakama Kuu jijini Dar baada ya Lulu kuachiwa, Dk. Cheni alisema kwa sasa anaanza mchakato wa kumsaidia Kajala mpaka ajue hatima ya kesi  inayomkabili.

“Unajua Lulu siyo mtu wa kwanza kumsaidia na mama yake ndiye aliniomba, nilishawasaidia wengi. 


Hata Cloud alipofungwa nilifuatilia mimi na Dude mpaka mwisho, hatukukata tamaa na kwa Kajala nitafanya hivyo kwa sababu ni mwenzetu jamani, naamini Mungu anaweza sana na atafanikisha kila kitu,” alisema Dk. Cheni.

Kajala anasota Segerea akikabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa bondi na serikali kutokana na mumewe kutakatisha fedha haramu.

TUPE MAONI YAKO

LULU MICHAEL AKATAA KUFANYIWA "SHEREHE" YA KUPONGEZWA KUINGIA URAIANI



January 29 2013 ndio msajili alithibitisha kwamba mwigizaji Lulu ametimiza masharti yote ya dhamana juu ya kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia na hivyo  kumwachia  kwa dhamana.....
 
Lulu na mama yake mzazi wote kwa pamoja waliangua vilio baada ya dhamana yao kukamilika wakati wakiwa nje ya Mahakama kabla ya kuondoka na Lulu kuingia uraiani.

Kabla  ya dhamana  hiyo kulikwa  na  tetesi  kwamba  Lulu angefanyiwa  sherehe kubwa  ya  kupongezwa  kuja uraiani.

Kwa mujibu wa ndugu yake  wa karibu, Lulu amegoma  kufanyiwa sherehe  na  badala  yake jana aliwaomba  watanzania  wamuombee  kwa  mungu  maana  kesi bado inaendelea.....
 
 “Nawashukuru watu wote na nilikua naomba watu waendelee kuniombea sababu hii ni dhamana tu lakini kesi bado ina safari ndefu… nawashukuru wale wote waliokua na mimi kwa hali yeyote ile na zaidi zaidi namshukuru sana Mwenyezi Mungu”....LULU
TUPE MAONI YAKO

"NIMEANDAA FILAMU MPYA AMBAYO NITAMSHIRIKISHA LULU MICHAEL"....JACKLINE WOLPER

MSANII wa filamu Tanzania Jackline Wolper ameandaa filamu mpya atakayoshirikiana na  msanii maarufu Elizabeth Michael 'Lulu' itakayokamilika hivi karibuni baada ya msanii huyo kutoka gerezani kwa dhamana

Akizungumza na Maisha Wolpa alisema amepata faraja baada ya taaratibu na sheria kufuatwa na hatimaye Lulu kuweza kupata dhamana hivyo anatarajia kufanya naye kazi ya filamu mpya itakayoanza kurekodiwa baada ya msanii huyo kufika uraiani

Alisema kuwa anatarajia atafanya vizuri katika filamu hiyo kwani tangu awali alikuwa akifanya vizuri katika tasnia hiyo ya uwigizaji kabla ya kupatwa na matatizo

"Nimeshampokea Lulu tangu moyoni mwangu kwani kule alikokuwepo si sehemu nzuri na ukiangalia bado ni mtoto mdogo hivyo inaumiza sana" alisema Wolper

Filamu hiyo ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuchezwa na Lulu baada ya kufika Uraiani

Wakati huo huo Rose Ndauka alisema ni wakati wa wasanii kumpokea mwenzao kwani wote ni familia moja na wanahitaji kushirikiana katika kila hali

Alisema kuwa ukiangalia umri wa msanii huyo ni mdogo hivyo ananafasi kubwa bado ya kutengeneza maisha yake na kuangalia wapi amekosea na wapi anapaswa kurekebisha

Naye msanii Single Mtambalike 'Richie Richie' alisema anashukuru kuona sheria imechukua mkondo wake na hatimaye sasa ameweza kuachiwa kwa dhamana hivyo kwa upande wao ni faraja kubwa kwani wote ni familia moja

Alisema anaamini sasa ataweza kujipanga na kufanya kazi vizuri kwani anakipaji na bado wanamuhitaji watanzania kulingana na uwezo mkubwa alionao kwenye tasnia hiyo
TUPE MAONI YAKO

CHOZI LA UCHUNGU LAMTOKA "LULU MICHAEL" BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI KWA DHAMANA...


 Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyumba akifuatiwa na mama yake mzazi.
 Wasanii nao wallijitokeza mahakamani hapo kumfariji Lulu, kulia ni msanii wa filamu, Muhsin Awadh 'Dk. Cheni'


Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyumba akifuatiwa na mama yake mzazi.


Baada ya jana kushindikana kwa sababu zisizo zuilika hatimaye msanii maarufu Elizbeth 'Lulu' Michael ametoka kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yote ya dhamana yake yaliyo tolewa na mahakama kuu.

Mara baada yakutoka Lulu alieyeonekana akiwa mwenye majonizi na furaha kiasi aliomba watanzania wote wamuombee maana hii ni dhamana tu na kesi yake bado inaendela. Ali washukuru watu wote waliokuwa pamoja nae katika mkasa huuu  amabao bado unamzunguka na pia alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa pamoja nae katika kipindi chote cha matatizo yanayo mkablia.

Wakili wake Ndugu Flugence Massawe amesema kwamba hii ni hatua ya kwanza kwasababu case bado inaendelea. Kwa sasa wanasubiri mahakama itoe tarehe ya Lulu kurudi mahakamani.
TUPE MAONI YAKO

PICHA ZA LULU MICHAEL AKIWA HURU URAIANI.....

 Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake.
Lulu akiwa ndani ya gari baada ya kukamilisha dhamana yake.
Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu.
Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.
Gari lililombeba Lulu likiondoka mahakamani.
Lulu akishuka katika gari la polisi baada ya kuwasili mahakamani leo.
Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana leo.
 --------------------------------
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha taratibu zote za dhamana.
TUPE MAONI YAKO

VIDEO YA YALIYOMKUTA LULU MICHAEL AKIWA MAHAKANI LEO.....


Furaha ya msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu kurejea uraiani baada ya mahakama kuu Dar es salaam kuridhia kupewa dhamana imeyeyuka kutokana na kurejeshwa rumande licha ya kukidhi vigezo vya dhamana vilivyotolewa na mahakama hiyo kutokana na kutokuwepo kwa msajili wa mahakama aliyetakiwa kupitia vielelezo vya dhamana.
TUPE MAONI YAKO

LULU AMERJESHWA RUMANDE BAADA YA TARATIBU ZA MAHAKAMA KUKWAMA....


Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo ofisini na hivyo kurudi rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana
Lulu akipanda gari la magereza.
Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani leo
 ---------------------------------------

Mahakama Kuu ya Tanzania leo  mchana  iliweka wazi masharti ya dhamana ya msanii  wa filamu anayejulikana zaidi kwa jina la Lulu,. ambaye jina lake halisi ni Elizabeth Michael.....


Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo mahakamani mchana , dhamana ya mwigizaji Lulu ipo wazi endapo tu angetimiza masharti yaliyotengewa ambayo ni

  • Kuwasilisha au kukabidhi hati yake ya kusafiria(passport)
  • Kutosafiri nje ya Dar es salaam.
  • Kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi
  • Kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atamdhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Pamoja na kwamba familia ya Lulu walikuwa wamejiandaa kukabiliana na kutimiza masharti hayo, Lulu amerudi rumande leo kutokana na kwamba  watumishi wawili wa serikali(Mahakama) ambao wanahusika na sehemu ya dhamana hiyo kwa upande wa sahihi za kimahakama, hawakuwepo Mahakamani hapo .....

 Hata hivyo, kwa mujibu wa mawakili wanaomwakilisha Lulu, masharti yote ya dhamana wameshayatimiza na kinachosubiriwa ni huo uthibitisho na utaratibu wa kimahakama ili Lulu arejee nyumbani na kuendelea kukabiliana na kesi hiyo akiwa uraiani.

Kwa maana hiyo, uwezekano ni wazi kabisa kwamba Lulu ataachiwa rasmi kesho January 29, 2013.
TUPE MAONI YAKO
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger