Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » KICHANGA CHAKUTWA KIKINING’INIA JUU YA MTI

KICHANGA CHAKUTWA KIKINING’INIA JUU YA MTI

tangazo

KATIKA hali isiyo ya kawaida, kichanga cha siku sita cha jinsi ya kike kimekutwa kimetelekezwa na mtu asiyefahamika juu ya mti ambapo kiliokotwa na mpita njia katika kijiji cha Losimingori kwa Laoshiye, wilayani Arumeru,  ambapo kilikuwa kumeviringishwa kwenye mfuko wa plastiki.

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Shongon Leswaki Mayo, kichanga hicho kilikutwa hivi karibuni saa 12 jioni na mpita njia aliyetajwa kwa jina la Neema Papalang wakati akipita eneo hilo na kushtuka kuona mtoto analia juu ya mti bila kuwepo mwangalizi yeyote.

Alisema baada ya tukio hilo, msamaria huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa eneo hilo mbapo yeye na viongozi wengine walifika na kushuhudia kichanga hicho ambapo kilionekana chenye afya njema.


Aidha, mtendaji huyo alisema kuwa haikufahamika mara moja mtu aliyehusika na  unyama huo wa kikitelekeza kichanga hicho ambapo pamoja na mambo mengine uongozi uliamua kumkabidhi mwanamke huyo kwa lengo la kukihudumia huku taratibu zaidi za kumsaka mama yake zikiendelea.


“Uongozi wa kijiji unaandaa utaratibu wa kukipeleka hospitali ili kuchunguza afya yake. Tukio hilo limewashtua wakazi wa eneo hili ambao ni jamii ya wafugaji,” alisema mtendaji huyo na kuongeza kuwa wanafanya msako katika eneo hilo na jirani kuweza kumbaini mwanamke yeyote aliyekuwa na ujauzito hivi karibuni na atakayebainika kufanya unyama huo atachukuliwa hatua za kisheria.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger