Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » TUNDAMAN ALIZWA MILIONI 7 NA "JIMAMA" WAKIWA FARAGHA

TUNDAMAN ALIZWA MILIONI 7 NA "JIMAMA" WAKIWA FARAGHA

tangazo

MSANII Tundaman baada ya kumcheka mwenzake Matonya na kumuimba kwenye wimbo wake kuwa alifungiwa ndani na mwanamke na kulizwa shilingi milioni 6, hali kwake imekuwa mbaya zaidi ambapo inadaiwa kuwa hivi karibuni amekombwa milioni 7 na mwanamke mmoja aliyelala naye na kujikuta akiwa hana hata chenji mfukoni.

Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na mwandishi kwa sharti la jina lake kutotajwa kilidai kuwa, msanii huyo alikuwa na sh milioni 7 ambazo alizipata kwenye moja ya show alizofanya hivi karibuni.


Mhabishaji huyo alisema kuwa baada ya kupata kiasi hicho cha pesa alisita kwenda kulala kwa rafiki yake Madee ndipo alipoamua kwenda kwa mwanamke huyo kwa lengo kutunza fedha hizo bila kuchukua tahadhari yoyote na fedha hizo, kitu ambacho kimempelekea kupoteza fedha zote huku mwenyewe akiwa kimya kwa hofu ya kuchekwa.


“Jamaa hadi leo kimya hafanyi tena mchezo wa kwenda kulala na demu na mshiko mrefu kwani kilichomkuta anajuta ni kwa nini alimuimba Matonya kwenye wimbo wake,” kilidai chanzo hicho.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger