Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » UTULIVU WAREJEA MTWARA BAADA A WANAJESHI WA JWTZ KUINGILIA KATI , ZAIDI YA WATU 40 WAKAMATWA

UTULIVU WAREJEA MTWARA BAADA A WANAJESHI WA JWTZ KUINGILIA KATI , ZAIDI YA WATU 40 WAKAMATWA

tangazo

Hali ya  utulivu  inadaiwa  kurejea katika wilaya ya Masasi  mkoani Mtwara baada ya   vikosi  vya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na  polisi  kuungana  kuweka ulinzi huku  watu  zaidi ya 40  wakikamatwa  kuhusika na matukio  ya vurugu za jana.

Mwandishi
John Kasembe  kutoka Mtwara anaripoti  kuwa kutokana na vurugu  hizo  waziri mkuu Mizengo Pinda na  waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi usiku  huu wapo Mtwara  wakiendelea na vikao  vya  kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.

Pia inadaiwa  mida ya asubuhi  leo  polisi  walilazimika  kutumia mabomu ya machozi  kuwatawanya  vijana ambao  walikuwa  wamefunga barabara na  kuwatoza ushuru  batili  wa shilingi 5000 wenye magari kama sehemu ya kujipatia fedha kwa njia feki.

Mbali ya tukio  hilo bado katika mitaa mbali mbali ya Mtwara  kwa siku ya leo shughuli  zote za uzalishaji mali zikiwemo biashara zimesimamishwa kwa  muda  ili  kukwepa vurugu kama za jana  japo shughuli za ibada  zimeendelea kwa  utulivu  zaidi.


TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger