tangazo
Ninauhakika utakua unaikumbuka ile stori ya mwimbaji wa bongofleva Stara Thomas kutangaza kuokoka na kuachana kabisa na muziki wa bongofleva, badala yake atakua anafanya gospel.
Japokua alitangaza kuwepo kwenye gospel rasmi baada ya kuokoka, Stara aliwahi kuweka wazi kwamba wasanii wa gospel hawana upendo na umoja, yani ni afadhali wasanii wa bongofleva mara mia manake amelishuhudia hilo kwa macho yake na wala sio kuhadithiwa.
Alichosema Linex ni kwamba wimbo huo wa bongo fleva umeshakamilika na kinachosubiriwa ni taratibu zilizopangwa za kuuachia, na kwa mujibu wa Linex ni kwamba Stara Thomas mwenyewe ndio alimpigia ili wairekodi hiyo kolabo ya bongofleva.