tangazo

Pistorius katikati akifikishwa mahakamani jijini Pretoria, akishtakiwa kwa mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Reeva Steenkamp enzi za uhai wake kabla ya kupigwa risasi na mpenzi wake Pistorius na kufariki dunia Siku ya Wapendao.

Pistorius akiwa katika moja ya mashindano ya mbio za walemavu alizokuwa akishiriki.
JO’BURG, Afrika Kusini
'Polisi
inaamini kuwa siri ya ujauzito aliyopewa ilimfanya Pistorius acharuke
na kuingia katika mabishano yaliyosababisha kifo cha Reeva – kwa kupigwa
risasi nne kichwani, kifuani, mkononi na nyongani'
MWANARIADHA
wa mbio za walemavu, Oscar Pistorius anayekabiliwa na shitaka la kumuua
mpenzi wake kwa risasi, amedaiwa kuwa huenda alimuua mwanamitindo huyo
wa zamani akiwa mjamzito.
Kama taarifa hizi
zitathibitishwa, itakuwa mfululizo wa madai unaomuweka nyota huyo kwenye
hatari ya kufungwa kifungo cha maisha – kwa kumuua mpenziwe Reeva
Steenkamp katika nyumba yake katika usiku wa kuamkia Siku ya Wapendanao.
Katika
utetezi wake wa awali, Pistorius alidai kumuua Steenkamp kwa bahati
mbaya, baada ya kuhisi amevamiwa na jambazi aliyejificha bafuni na
kwamba kwa kuwa hakuwa na miguu yake ya bandia, hakuona njia ya kujihami
zaidi ya kufyatua risasi mfululizo.
Ni utetezi uliopingwa na waendesha mashtaka wa kesi hiyo – waliodai kuwa tukio limefanyika kwa makusudi baada ya mabishano.
Taarifa
zilizochapishwa juzi Jumatatu na gazeti la National Enquirer la hapa
zimedai kuwa, huenda mabishano baina ya wawili hao yalitokana na habari
kuwa Pistorius alikuwa akikaribia kuitwa baba wa kichanga cha mrembo
huyo.
Chanzo cha karibu na uchunguzi
kililiambia gazeti la udaku kuwa: 'Polisi inaamini kuwa siri ya ujauzito
aliyopewa ilimfanya Pistorius acharuke na kuingia katika mabishano
yaliyosababisha kifo cha Reeva – kwa kupigwa risasi nne kichwani,
kifuani, mkononi na nyongani.'
Chanzo hicho kiliongeza kuwa: 'Baadaye usiku, majirani walisikia mabishano yaliyofuatiwa na ufyatuaji risasi katika nyumba yao.
'Polisi
waliitwa kwa uchunguzi, lakini walijiridhisha tu kuwa ulikuwa ubishani
wa kimapenzi, hivyo hawakuwa na uchunguzi wa maana waliotarajiwa
wangeulizwa kuhusiana na sakata hilo.'
Likiambatanisha
na picha iliyopigwa siku chache kabla ya kifo cha Reeva, gazeti hilo
limeripoti wasiwasi huo, sambamba na habari kuhusu ibada maalum ya
kumuombea marehemu aliyoandaa Pistorius nyumbani kwa mjomba wake
anakoishi kwa sasa.
Habari mseto via Daily Mail