Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » HATIMAYE MRITHI WA PAPA BENEDICT WA 16 APATIKANA

HATIMAYE MRITHI WA PAPA BENEDICT WA 16 APATIKANA

tangazo

Jorge Mario Bergoglio(Pope Francis) akipewa salamu na Papa aliyejiuzuru Benedict 16



Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa. Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I. Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa.
 Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao. Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki. Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.


Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya. Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa. 

Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne. Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger