Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » IDADI YA WAETHIOPIA YA WALIOFARIKI WAFIKIA WATANO

IDADI YA WAETHIOPIA YA WALIOFARIKI WAFIKIA WATANO

tangazo

Idadi ya vifo vya Waethiopia waliokamatwa Machi mosi, mwaka huu, katika maeneo ya Kitumbi Barabara ya Segera-Chalinze wakiwa ndani ya makontena wakisafirishwa kutoka jijini Arusha kuelekea jijini Dar es Salaam imefikia watano hadi sasa.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, COSTANTINE MASSAWE amesema wahamiaji hao walikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na walikutwa mmoja akiwa amefariki dunia kwa kukosa hewa huku saba wakiwa hawajitambui.

 
Kamanda MASSAWE, amesema wahamiaji hao ambao wako 54 walichanganywa na mzigo wa Nondo na baada ya magari yaliyowabeba kukamatwa madereva wa magari hayo mawili walitokomea kusikojulikana wakihofia kukamatwa ambapo hadi sasa majina yao hayajatambulika.

 
Aidha Kamanda MASAWE, ameiomba jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa kuhusiana na vitendo vya aina hiyo ili viweze kudhibitiwa.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger