Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MAKALIO YA AUNT LULU YASABABISHA NJEMBA IDONDOKE CHINI NA KUZIMIA

MAKALIO YA AUNT LULU YASABABISHA NJEMBA IDONDOKE CHINI NA KUZIMIA

tangazo

Njemba ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amenusurika kifo kufuatia kuanguka ghafla na kupoteza fahamu kwa madai ya kuchanganywa na mauno ya Aunty Lulu

Mkasa huo ulijiri kwenye sherehe ndogo ya watu wa karibu baada ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kufunga ndoa na Gardner Dibibi, Kinondoni, Dar es Salaam wiki iliyopita.





Ilikuwa ni wakati wa ndugu, jamaa na marafiki wakipata msosi sanjari na vinywaji huku muziki ukipigwa nyumbani kwa familia ya bibi harusi, Kinondoni, ndipo Aunty Lulu alipoanza kukata mauno na kushangiliwa.


Wakati watu wakimpa dole Aunty Lulu, jamaa huyo alimtolea macho pima na kuanza kuchanganyikiwa na mauno hayo.


Polepole jamaa, mkono mmoja ukiwa umeshika sahani yenye msosi mwingine soda, aliganda kwa sekunde kadhaa kama vile haamini anachokiona.


Kufumba na kufumbua, njemba alikwenda chini ghafla na kupoteza fahamu.


Hali ya hewa ilichafuka kuanzia hapo, ikawa patashika nguo kuchanika.


Hata hivyo, wanaume majasiri waliokuwa eneo la tukio walimpepea jamaa huyo ambapo baadaye alizinduka. 

  
Jamaa huyo baada ya kurejewa na fahamu alisikika akisema: Ukweli wowowo la huyu dada (Aunty Lulu) limenichanganya, nusu linitoe roho jamani.


Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kilichomtokea jamaa huyo ni mfadhaiko
.

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger