Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MSANII RADO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPOKEA KICHAPO KIKALI MWANANYAMALA

MSANII RADO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPOKEA KICHAPO KIKALI MWANANYAMALA

tangazo


MSANII wa muziki na filamu Bongo, Saimon Mwapagata ‘Rado’ amenusurika kifo kutoka kwa vijana waliofunga njia maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar Jumapili iliyopita. 



Kwa mujibu wa rafiki wa Rado ambaye pia ni msanii wa filamu, Deogratius Shija, tukio hilo lilitokea usiku wakati Rado alipokuwa akirudi nyumbani kwake...

“Alikuta njia imefungwa na vijana watatu, alijaribu kuwapigia honi lakini hawakufungua njia.

“Rado alishuka kwenye gari na kuwauliza kwa nini wamefunga njia wakamjibu kwamba mmoja wao ameibiwa simu, hivyo wanamtafuta mwizi wao.
Shija alisema kwamba ghafla vijana wale walimvamia Rado  na kumshushia kipigo cha haja wakiwa na mapanga na marungu na kumjeruhi hadi akapoteza fahamu.

 “Nilipigiwa simu na msamaria  na kuambiwa kuwa Rado hajiwezi, sababu kuna watu wanaomjua maeneo yale alipelekwa Oysterbay Polisi kisha kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala ambako alishonwa, kifuani na mguuni,”


TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger