Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MUUMIN AREJEA TENA KWA KISHINDO....

MUUMIN AREJEA TENA KWA KISHINDO....

tangazo

Hatimaye bendi ya Victory Sound imezinduliwa rasmi jana katika ukumbi wa Mango Garden, bendi hiyo ilipanda jukwaani na kuanza kuonyesha shoo ambayo iliandaliwa kwa ajili ya mashabiki wake

Hakika uingiaji wa bendi hii kwenye jukwaa ulikuwa wenye ubunifu,ambapo ulikumbusha baadhi ya mashabiki wakati  Muumin alipoizindua Bwagamoyo Sound katika ukumbi wa Vatican Hotel Sinza miaka kadhaa iliyopita.

Mashabiki wa bendi hii ambao walijitayarisha kwa mambango na sharashamra nyingi waliongeza uchangamfu katika uzinduzi huu. Kwa mara nyingine tena Waziri Sonyo alionekana jukwaani akiwa na ule uimbaji wake wa sauti ya juu kuonyesha kuwa bado anakipaji cha uimbaji.

Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo Muumini atatakiwa ayazingatie ili kujiweka sawa katika mpambano huu aliyojikita. Kwanza lazima kufanyia kazi tatizo sugu la kukosekana kwa muziki ulio balanced, mafundi mitambo wengi hudhani vyombo kulia kwa nguvu ndio kuonyesha ubora wa ufundi wao, kinachotokea ni kelele ambazo hufanya kusikiliza muziki inakuwa adhabu badala ya starehe.

Pili ni lazima afanye tena mabadiliko katika muziki wake kwani bado unafanana sana na bendi ambazo ziko hewani, hili ni jambo la hatari kwani watu wanaweza kuona hakuna jipya kimuziki. Wacheza show watalazimika kufanya mazoezi makali ili kujifua zaidi.


Credit: pro24
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger