Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MWANAMKE AKAMATWA AKIWAUZA WATOTO WAKE FACEBOOK ILI APATE HELA YA KUMUWEKEA DHAMANA MCHUMBA WAKE

MWANAMKE AKAMATWA AKIWAUZA WATOTO WAKE FACEBOOK ILI APATE HELA YA KUMUWEKEA DHAMANA MCHUMBA WAKE

tangazo

Mwanamke mmoja huko Oklahoma ameshitakiwa kwa kujaribu kuwauza watoto wake ili apate fedha za kumuwekea thamana mchu wake.
 
Polisi katika mji wa Wallisaw wamesema mwanamke huyo Misty VanHorn aliwasiliana na mnunuzi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
 
Wamesema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa akitaka dola 1,000 kwa mtoto wake mwenye miaka miwili au dola 4,000 kwa mtoto wake mdogo mwenye miezi 10.
 
Anadaiwa kuandika katika face book akimuelekeza mnunuzi kuwa afike Sallisaw na atamkabidhi mtoto pamoja na vitu vyake vyote na kumuachia moja kwa moja.
 
Mwanamke huyo mnunuzi ambaye hajajulukana anayeishi jimbo la jirani la Arkansas alitoa taari kwa mamlaka za jimbo hilo.
 
Polisi walifika eneo hilo na kumkamata Misty VanHorn mara moja.
 
Majirani zake wamesema VanHom amekuwa akitembea mlango kwa mlango akijaribu kuchangisha dola 1,000 ili kumtoa mwenzi wake kwa dhamana.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger