Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » "TUMEKUWA TUKILEA MTOTO MCHAWI KWA MUDA MREFU BILA KUJUA".....NIKITA WA BONGO MOVIE

"TUMEKUWA TUKILEA MTOTO MCHAWI KWA MUDA MREFU BILA KUJUA".....NIKITA WA BONGO MOVIE

tangazo
 KELVIN....

STAA wa filamu za Kibongo, Ahmed Khalfan ‘Kelvin’ na mkewe mwigizaji, Elizabeth Chijumba ‘Nikita’ wamesema mmoja wa watoto pacha waliowaasili (adopt) mwenye umri wa miaka sita, ameonesha matendo ya kichawi...
 

Akizungumza na mwandishi wetu, Kelvin alisema waliwachukua watoto hao mapacha kwa bibi yao Mtwara mwaka 2009 kwa lengo la kuwalea kutokana na mazingira magumu waliyokuwa nayo lakini walipofika Dar, mmoja alianza kuonesha vitendo tofauti vya kichawi.

“Wakati tukiendelea kuishi nao, tulimuona mmoja ana vitukovituko mara kwa mara na tuligundua kuwa mke wangu alikuwa akiumwaumwa kila alipomgombeza mtoto huyo.

“Kuna siku niliamka usiku kwenda kwenye chumba walichokuwa wakilala watoto hao, nikamkuta akiwa uchi akirukaruka kitandani na nilipomshtua alijilaza kitandani na asubuhi tulipomuuliza, alisema muda ule bibi yake alikuwa akimrudisha kutoka kuroga Tanga."

Kwa upande wake, Nikita alipomdadisi mtoto huyo kuhusu vitendo hivyo vya kichawi, alimwambia kuwa bibi yake anataka kumuua kwa sababu wanamzuia asirudi kijijini kwao Mtwara akaendelee kufanya kazi za kichawi. 

“Kwa kweli nampenda sana lakini sina budi kumrudisha nyumbani kwao, roho inaniuma kwa sababu nilimzoea,” alisema Nikita.

Mwandishi wetu alipomuuliza mtoto huyo kuhusiana na sakata hilo, alikiri kuwa ni kweli bibi yake ni mchawi na huwa anamchukua kwenda sehemu mbalimbali kuroga kwa kutumia usafiri wa ungo na ndiye anayemroga Nikita.

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger