tangazo
Habari:
Kila nikiwa na nyoa nywele sehemu za siri baada ya siku kama mbili
natokewa na vipele ila kina kuwa kimoja kimoja vinaweza kutoka vipele
kama vitatu baadaye kama baada ya wiki kama moja vinaisha je ni tatizo?
au? maana vinaninyima raha?
Na huwa sirudii shavingmachine nikitumia
mara moja basi.. Je nitatizo au sababu iko wapi na naomba unishauri
nitumie dawa gani...
Jibu langu:
Tumia "after Shave" mara baada ya kuondoa nywele hizo. Nyele za
kiafrika zimejiviringa/nyonga (curl) hivyo basi unapozinyoa unatakiwa
kunyoa na mizizi yake na njia pekee yakufanya hivyo kuhakikisha eneo
zima la nywele limelainishwa kwa povu lakutosha la sabuni inayoendana na
ngozi yako au "shaving cream" ambayo pia imetengenezwa maalumu kabisa
kwa ajili ya aina ya ngozi yako.
Povu la sabuni au "shaving cream" inapopakwa kwenye nywele huingia mpaka kwenye mizizi na kuilainisha na unapopitisha uwembe unakuwa umenyoa nywele zote kutoka mzizini na sio kukata nywele hizo kwa juu-juu tu tendo ambalo husababisha vipele pale nywele zinapoanza kuota tena. Kumbuka kunyoa kila baada ya wiki mbili na usirudie wembe ikiwa unatumia ndio kifaa utumiacho.

Nakaribisha maoni