Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » HALI NI MBAYA HUKO BOSTON : DA' CHEMI ASIMULIA JINSI WALIVYOAMRIWA WASITOKE NJE NA JINSI HALI ILIVYO

HALI NI MBAYA HUKO BOSTON : DA' CHEMI ASIMULIA JINSI WALIVYOAMRIWA WASITOKE NJE NA JINSI HALI ILIVYO

tangazo
Nimeamshwa na simu kutoka Emergency Alert ya mji wa Cambridge , MA wakisema kuwa ni maarufu kutoka nje ya majumba yetu leo! Hakuna usafiri, wameomba sehemu za kazi zisifungue!

Wanasema kuwa hakuna kufungua mlango hata kama ni polisi, wanasema kuwa jamaa anataka kuua watu!

Jana usiku ilikuwa balaa hapa Cambridge! Cambridge ni nje ya Boston.  Kwanza kwenye saa tatu na nusu (9:30PM) tulisikia kuwa majambazi walivamia duka la  7-11 Central Square!

 Kukaa kidogo tukasikia Polisi kapigwa risasi Chuo Kikuu cha MIT! Baada ya muda mfupi wakasema yule polisi kafa!

Kwenye saa tano tukasikia mtu kaibiwa gari yake aina ya Mercedes Benz, kwenye kituo cha mafuta!  Ni mwendo mfupi toka ninapokaa! Nikaanza kusikia milio ya gari ya polisi!

Kumbe polisi wa kila aina walikuwa wanawafukuza  karibu na Arsenal Mall. Milio ya risasi balaa, ambulance na magari ya polisi yalikuwa yanafukuzana, kwenye TV, tukaona kila mtu aliyefanana na Mspanish, Mwarabu kasimamishwa na kusachiwa!

Sikulala hadi saa nane na nusu! Nimeamshwa na simu ya Emergeny Alert!

Duh, hii ni kama SINEMA!

Wanasema huyo gaidi wanayetamfuta anaitwa Zohkar Sarnev  mwenye miaka 19, anatoka Chechnya! Huyo gaidi wanayemtafuta, nilikuwa nawaona hapa Cambridge lakini nilidhani ni wanafunzi wa kawaida!

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger