tangazo
Lucy Komba actress mwenye jina kubwa Swahiliwood anakuja kivingine katika filamu mpya inayoitwa "From Tanzania To Denmark" ambayo imetengenezwa katika nchi hizi mbili huku ikishirikisha waigizaji wa Tanzania na wengine kutoka Denmark ambao wengine wana asili ya kiafrika na wengine asili ya Denmark. Waigizaji hao ni kama Selembe Toko na Maggie Moreno.
Filamu inahusu binti mmoja(Lucy Komba) kutoka kijijini
anakuja Dar es salaam ili aende Denmark lakini kutokana na vituko vyake
akiwa mshamba wa kupitiliza ndiyo itakufanya uwe na hamu ya kuitizama
filamu hii ili umuone binti huyo atakuwaje na ushamba wake huko
Debnmark kama akiwa Dar-es salaam tu anafanya drama za kufa mtu.
Lucy
now yupo katika maandalizi ya kwenda Denmark ambapo filamu hii
itazinduliwa huko ambapo ameshirikiana na kampuni ya Vad Production
katika kuiandaa na tayari imeshakamilika. Kaa mkao wa kula usikose
filamu hii
Mbali na balaa hilo, Vad Production imekwisha kamilisha filamu yake mpyaaaa iitwayo "IF I KNEW" ambayo itaingia sokoni siku ya jumatatu....
Filamu hiyo ya kimataifa imewashirikisha wakali wa filamu duniani kama SAFARI LUKEKA ,TANTINE DANIEL MUSA, FRANK SALUMU na ELIANE KISONGA
Kazi kwao mdau wa filamu.
HII NI TRAILER YA FILAMU HIYO
Credit:<< Vadfilm production>>