Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MKE WA MTU AKUMBWA NA BALAA NA MSAKO WA MACHANGUDOA

MKE WA MTU AKUMBWA NA BALAA NA MSAKO WA MACHANGUDOA

tangazo

MKE wa mtu ambaye jina lake halikufahamika mara moja (pichani),hivi karibuni yalimkuta makubwa baada ya kuibiwa vitu vyake vyote vilivyokuwa ndani ya pochi na dereva wa Bajaj ambaye pia jina lake halikufahamika.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo dada huyo alikodi Bajaj hiyo toka nyumbani kwake, Kinondoni-Shamba jijini Dar kwenda kujirusha katika klabu moja ya usiku iliyopo Mwananyamala ndipo alipolizwa pochi hiyo iliyokuwa na fedha (zaidi ya elfu hamsini) pamoja na vitambulisho.


Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, kabla hajafika klabu, dada huyo aliamua kumpitia shosti yake aliyekuwa katika Baa ya Uhuru Peak, Mwananyamala ili wakajirushe pamoja ndipo dereva huyo alipomfanyizia.
 

 “Alipofika hapa Uhuru Peak akaacha pochi yake ndani ya Bajaj ili amshtue fasta rafiki yake ndipo dereva alipotumia mwanya huo kutokomea kusikojulikana,” kilisema chanzo hicho. 

 Baada ya dakika kadhaa, dada huyo alitoka nje na kuanza kuangaza huku na huko ghafla akapata msala mwingine wa kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi lililokuwa katika msako wa kuwakamata machangudoa.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger