Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » BAHATI BUKUKU APATA MCHUMBA MWINGINE BAADA YA KUZINGUANA NA MUMEWE ....

BAHATI BUKUKU APATA MCHUMBA MWINGINE BAADA YA KUZINGUANA NA MUMEWE ....

tangazo


MWIMBAJI wa Muziki wa Injili , Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa talaka yake


Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia Haina Huruma aliweka wazi kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Basila.
 

Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.


Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.
 

Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger