Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » "NDOTO ZANGU NI KUOLEWA NA MSANII AY"....SALAMA JABIR

"NDOTO ZANGU NI KUOLEWA NA MSANII AY"....SALAMA JABIR

tangazo
 
Mtangazaji mahili wa show za TV/Radio aliyeisimamisha wima show mpya na kali inayorushwa kupitia channel 5 ‘Mkasi’ namzungumzia Salama Jabir ametupia ‘neno’ kupitia kipindi hicho kuwa huenda siku moja akaolewa na AY!



Kama uliiangalia show ya Mkasi jumatatu ama marudio yake leo (jumamosi) ambapo crew nzima ya kipindi cha mkasi chini ya C.E.O na Producer wa show Ambwene Yesaya ‘AY’ walikuwa wakieleza changamoto na mambo mbalimbali waliyokutana nayo wakati wanaanza kufanya kipindi hicho, mwishoni Salama ambae alikuwa akimuelezea AY kuwa ni msanii ambae anajivunia kufanya nae kazi kutokana na jinsi alivyomchapakazi na mtu wa kuaminika alimaliza kwa kusema “huenda ipo siku moja tutaona..!”.



Wote tunajua Salama  alivyo mtu wa utani sana, kitu kinachoongeza burudani ya ziada katika show zake, alitamka hivyo na kumgeukia AY akimuuliza, na AY mwenyewe akajikuta anacheka na kukubali.

Pengine ulikuwa ni utani tu, lakini hakuna aijuae kesho ukizingatia wote wako single!



TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger