Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA , BUXTON CHIPETA AFARIKI DUNIA

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA , BUXTON CHIPETA AFARIKI DUNIA

tangazo


Jaji Buxton Chipeta.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu Tanzania, Buxton Chipeta amefariki dunia muda mfupi uliopita.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia, Jaji Chipeta alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari ambapo ilifikia wakati akalazimika kukatwa vidole kadhaa vya miguuni.

Enzi za uhai wake, Jaji Chipeta aliweza kujijengea heshima katika kazi yake na kufikia kuwa mmoja wa majaji wanaoheshimika mno hapa nchini.
 

Pia Jaji Chipeta aliwahi kuwa miongoni mwa majaji wa Tume ya kurekebisha Sheria yeye akiongoza kanda ya Dar es Salaam.
 

Mpekuzi  inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger