Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MAHAKAMA YAWAACHIA HURU VIONGOZI WA CHADEMA BAADA YA MWIGULU NCHEMBA KUSHINDWA KUTHIBITISHA AINA YA TUSI ALILOTUKANWA

MAHAKAMA YAWAACHIA HURU VIONGOZI WA CHADEMA BAADA YA MWIGULU NCHEMBA KUSHINDWA KUTHIBITISHA AINA YA TUSI ALILOTUKANWA

tangazo
Mwita  Waitara
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mjini Singida  jana imetupilia mbali kesi iliyokuwa inawakabali viongozi wawili wa CHADEMA Ndugu Mwita Waitara ambaye ni afisa sera na utafiti makao makuu na mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo. 
 
Katika hukumu yake aliyeiyosoma mbele ya wakili wa washtakiwa hao Tundu Lissu, hakimu wa Mahakama hiyo Masham alisema kuwa washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa. 

Aidha, hakimu huyo alisema kwamba upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchemba aliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yamemuathiri. 

"Kushindwa kwa Mwigulu Nchemba kufika mahakamani ni kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote alilotendewa na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa".. alisema hakimu huyo.  

Washtakiwa walidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 14 Julai mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago wilayani Iramba ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilikuwa na mkutano wa hadhara. 

Kesi hiyo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara, jambo ambalo lilikuwa likimkera hakimu wa kesi hiyo.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger