Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » "NIMECHOSHWA NA WANAUME MASHAROBARO WA TANZANIA....BORA WA NIGERIA WANAJUA KUPENDA"...REHEMA FABIAN

"NIMECHOSHWA NA WANAUME MASHAROBARO WA TANZANIA....BORA WA NIGERIA WANAJUA KUPENDA"...REHEMA FABIAN

tangazo

Mlimbwende  aliyewahi kung’ara katika Shindano la Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kuangukia kimapenzi kwa mtoto wa Balozi wa Nigeria nchini China aliyemtaja kwa jina moja la Allen anayetaka kufunga naye ndoa. 


Akichati na mwandishi wetu, kwa njia ya mtandao, Rehema alikiri kuwa na mwanaume huyo ambaye ni mtu mzima na kweli ni mtoto wa balozi huyo.
 


“Nimechoshwa na masharobaro hivyo nimeamua kutulia na mwanaume huyo kwa sababu nimempenda na yeye anaonekana kunipenda,” aliandika Rehema.

Rehema ambaye kwa muda mrefu amekuwa nchini humo, alisema kwamba amekuwa akipata wanaume wanaomtumia na kumuacha lakini safari hii amepata mtu sahihi.

“Tumepanga kuja Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mipango ya ndoa, hivyo nitarajieni huko muda si mrefu,” aliandika Rehema na kuongeza kwamba atafanya bonge la sherehe.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger